Fidiya na hady
Kwanza: Fidia
Maana ya fidiya
Ni kitu kinachomlazimu mwnye kuhiji au mwenye kufanya Umra kwa sababu ya kuacha tendo la wajibu au kufanya tendo lililokatazwa
Kwanza: Fidia ya kuacha tendo la wajibu
Mwenye kuacha wajibu miongoni mwa wajibu za Hija au Umra, kama aliyeacha kulala Muzdalifa au kunyoa au nyinginezo, itamlazimu fidia, nayo ni kuchinja mnyama.
Na mnyama anayekusudiwa ni fungu moja kati ya mafungu saba ya ngamia au ng›ombe au ni mbuzi aliyemaliza mwaka mmoja au kondoo aliyepita miezi sita. Atachinja katika Haramu ya Makka na nyama yake atagawia mafukara wa Makka.
Akikosa mnyama wa kuchinja, atafunga siku kumi: siku tatu akiwa Hija ikiwezekana, na siku saba arudipo kwa watu wake. Mwenyezi Mungu U Anasema: {Asiyepata (cha kuchinja) atafunga siku tatu huko Hija na siku saba mtakaporudi. Hizo siku kumi kamili. Hukumu hiyo ni kwa yule watu wake si wakazi wa eneo la Msikiti wa Haram. Na mcheni Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kutesa} [2: 196].
Pili: Fidia ya kufanya tendo lililokatazwa
1. Fidia ya kuvaa nguo ya mzunguko, kufinika kichwa, kujitia manukato, kunyoa nywele na kukata kucha.
Mwenye kufanya mojawapo ya matendo haya atachaguzwa baina ya mambo matatu:
a. Kufunga siku tatu.
b. Kuwalisha masikini sita, kila masikini nusu ya pishi ya chakula kama mchele na mfano wake.
c. Kuchinja mbuzi.
Dalili ni neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Na msinyoe vichwa vyenu mpaka wanyama waliotunukiwa kwa ibada ya Hija wafike mahali pa kuchinjwa. Basi mtu atakayekuwa mgonjwa, au ana vitu vya kumkera kichwani mwake, atatoa fidia ya kufunga, kutoa sadaka au kuchinja} [2: 196].
Na neno la Mtume (saw) kumwambia Ka’b bin ‘Ujrah t na yeye yuko kwenye ihramu: (Je, hao niwadudu wa kichwani mwako?). Akasema: “Ndio”. Mtume (saw) akamwambia: (Nyoa kichwa chako kisha uchinje mbuzi ikiwa ni ibada au funga siku tatu au lisha masikini sita pishi tatu za tende).
Mwenye kufanya katazo miongoni mwa makatazo matano yaliyotajwa kwa kukusudia, au akahitaji kulifanya na akalifanya, kama ilivyotokea kwa Ka’b t, basi atatoa fidia ya kero.
Na mwenye kufanya lolote miongoni mwa haya yaliyokatazwa kwa kusahau, basi hana makosa
Kunyoa nywele
Kukata kucha
Kujipaka manukato
Kuvaa nguo ya kushonwa
Kufunika kichwa kwa kitu cha kushika
Comments
Post a Comment