HOJA JUU YA KUWEPO KWA ARRABU
Ulimwengu Wote Wakiri Na Kukubali Na Kuamini Bali Hata Kusema Kuwepo Kwa Allah Mwenye Nguvu Na Utukufu. Asema Allah Mtukufu: {Mitume Wao Wakasema;”Je! Mnamfanyia Shaka Mwenyezi Mungu. Muumba WA Mbingu Na Ardhi? Yeye Anakuiteni Akusameheni Dhambi Zenu Na Akupeni Muhula Paka Muda Uliowekwa.”Wakasema:”Hamkuwa Nyinyi ILA Ni Watu Kama Sisi.Mnataka Tu Kutuzuilia Na Yale Waliokuwa Wakiyaabudu Baba Zetu. Basi Tuleteeni Hoja Zilizo Wazi} (Ibrahim: 10)
Muumini WA Kweli Ni: Yule Aliyeyakinisha Kuwa Allah Mungu Aliye Na Uwezo, Na Akayakinisha Kuwa Yeye Tu Ndiye Yuwafaa Kuabudiwa.
Vipi Wanataka Hoja Naye Allah Ni Hoja Tosha Kwani Yeye Ni Hoja Kwa Kila Kitu Kwa Nguvu Zake Na Uwezo Wake.
Huwezi Kumsifu Allah Isipokuwa Kwa Fadhila Zake Na Neema Zake, Nawe Kwa Hali Zote Una Muhitaji Allah Mwenye Nguvu Na Utukufu.
Hata Kama Tukiacha Haya Na Kuleta Hoja Za Kuthibitisha Kuwepo Kwake Allah; Tunapata Hoja Nyingi Tu Miongoni Mwazo:
HOJA ZA KIMAUMBILE
Allah... Ni Jina Lililonakshiwa Kwenye Umbile La Mwanadamu Kwa Hiyo Halihitaji Dalili Nyengine Nzito Zaidi Ya Hii.
Viumbe Waliumba Kwa Kawaida Wamuamini Allah Aliye Waumba, Ukawaida Huu Hauondoki ILA Kwa Mtu Aliyemfuta Na Kumuondoa Allah Kutoka Kifuani Kwake Na Akilini Mwake. Na Miongoni Mwa Dalili Kuu Zinazo Tuonesha Hivyo Kwamba Kawaida Na Maumbile Yana Kubaliana Na Kuwepo Kwake Allah Ni Maneno Yake Mtume (S.A.W) &" Kila Mtu Anazaliwa Na Maumbile Ya Dini Ya Kiislamu Lakini Wazazi Wake Ndio Humbadilishia Dini Wakamfanya Akawa Myahudi Au Mkristo Au Mwenye Kuabudu Moto, Kama Vile Mnyama Anavyo Zaliwa Masikio Yake Huwa Yako Sawa. Je! Mliwahikuona Mnyama Kazaliwa Masikio Yamekatwa? &"(Imepokewa Na Bukhari)
chanzo:
Comments
Post a Comment