Itikafu(kukaa ndani ya msikiti)

Maana ya Itikafu

Itikafu ki-lugha.
Ni kujilazimisha na jambo fulani, na kujifunga nafsi yako juu ya kulifanya jambo hilo.
Itikafu ki-sheria.
Ni kujilazimisha kukaa ndani ya msikiti kwa ajili ya kumuabudu Mwenyezi Mungu.

Usharia wa Itikafu

Kufanya itikafu ni katika matendo yaliyo bora sana, na twa’a tukufu. Kutoka kwa A’isha Mungu awe naye radhi anasema: “Alikuwa Mtume (saw) akifanya itikafu (maisha yake) katika kumi la mwisho wa mwezi wa Ramadhani mpaka Mungu alipomkabidhi roho yake (Mtume alipokufa)” [Imepokewa na Bukhari.].
Na inaruhusiwa ki-sheria kwetu sisi na kwa waliokuja kabla yetu kufanya itikafu, Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: ( Na tulimusia Ibrahimu na Ismaili Itakaseni nyumba yangu kwa ajili ya wale wanaoizunguka kwa ajili ya kutufu na wanaokaa hapo na (kwa ajili ya) wanaorukuu na kusujudu hapo pia”) ( Al-Baqarah –Aya 125).

Hukumu ya Kukaa Itikafu

Kufanya itikafu ni sunna wakati wowote ule, na ubora wake zaidi kuifanya ni katika kumi la mwisho wa mwezi wa Ramadhani; kwasababu Mtume ﷺ alidumu katika kufanya itikafu kwenye kumi la mwisho wa mwezi wa Ramadhani [Zaadul-Ma’ad.].

Comments

Popular Posts