JE, WATU WANA HAJA NA MITUME?

JE, WATU WANA HAJA NA MITUME?

Uchovu wa akili

Mwenyezi Mungu ameumba viumbe wake katika umbile (fitra) sahihi, na akawawekea akili ili waweze kupambanua baina ya haki kwenye batili, na kwa sababu akili za wanadamu zina mapungufu na udhaifu, matamanio na maslahi, bali na migongano ndani yake.
Katika hali hiyo wanachokiona baadhi ya watu kuwa ni kizuri na wema wengine wanaweza kukiona kuwa kibovu, bali hata mtu mmoja anaweza kubadilika rai yake kwa kubadilika kwa zama na mahali, pamoja na kuwa akili hizo haziwezi kudiriki kilichojificha katika hali halisi katika elimu mbali mbali, kadhalika hawezi kudiriki muradi wa Muumba, maamrisho yake na makatazo yake, mbali na kuwa mwanadamu hawezi kupokea kutoka kwa Allah moja kwa moja, Allah amesema: “Na haikuwa kwa mwanaadamu kwamba Mwenyezi Mungu amsemeze ila kwa Wahyi (Ufunuo), au kwa nyuma ya pazia, au kumtuma Mjumbe. Naye humfunulia ayatakayo kwa idhini yake. Hakika Yeye ni Mtukufu, Mwenye hikima. ” (42:51)
Hivyo basi Allah akachagua viumbe vyake bora zaidi miongoni mwa Mitume na Manabii ili wawe mabalozi wazuri baina yake Yeye Allah na waja wake, Allah amesema: “Mwenyezi Mungu huteuwa Wajumbe miongoni mwa Malaika na miongoni mwa watu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (22:75),
Ili wawaongoze watu katika kumuabudu Yeye, na wawaondoshe kwenye dhuluma za kiza na kuwapeleka katika uongofu wa Nuru, ili watu wasiwe na hoja kwa Allah baada ya kupelekewa Mitume –Allah amesema: “Mitume hao ni wabashiri na waonyaji, ili watu wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kuletewa Mitume. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima. ” (4:165).

Comments

Popular Posts