Kutawadha
Maana ya Kutawadha
Uzuri na usafi
Kutumia maji kwenye viungo maalumu kwa nia ya kujitwahirisha
Hukumu ya kutawadha
Kutawadha: ima ni lazima na ima inapendekezwa:
a. Ni lazima kutawadha kwa mambo matatu
1. Kuswali
Mwenyezi Mungu U Anasema: {Enyi Mlioamini! Mnapo simama kwa ajili ya swala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni} [5: 6]
2. Kutufu Alkaba:
Kwa kauli yake Mtume ﷺ kumwambia mwanamke aliye katika hedhi: (Usitufu mpaka utwahirike) [ Imepokewa na Bukhari.].
3. Kushika Msahafu:
Kwa neno lake Mwenyezi Mungu U: {Hawaigusi isipokuwa wale waliotwahiriwa} [56: 79]
b. Kutawadha kunasuniwa katika mambo mengine yasiyokuwa hayo
Kwa neno lake Mtume ﷺ aliposema: (Hajilazimishi na udhu isipokuwa mwenye Imani) [ Imepokewa na Ahmad].
Na kunapendekezwa zaidi kutawadha wakati wa kujadidisha udhu kwa kila Swala, kutawadha kwa kumtaja Mwenyezi Mungu na kuomba, wakati wa kusoma Qur’ani, kabla ya kulala, kabla ya kuoga, na kutokana na kumbeba maiti na baada ya kila tukio la kutangua udhu, hata kama hataki kuswali.
Fadhila za kutawadha
1. Ni sababu ya kupendwa na Mwenyezi Mungu
Mwenyezi Mungu aliyetukuka Anasema:{Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wenye kutubia na anawapenda wenye kujitwahirisha} [2: 222].
2. Ni alama ya umma wa Mtume Muhammad ﷺ kwa kuwa watakuja Siku ya Kiyama wakiwa weupe wa nyuso na viungo vya kutawadha
Amesema Mtume ﷺ (Hakika ya umma wangu watakuja Siku ya Kiyama wakiwa weupe nyuso na viungo kutokana na athari ya kutawadha, basi yoyote miongoni mwenu anayeweza kurefusha weupe wake na afanye) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
3. Kunafuta dhambi na makosa
Amesema Mtume ﷺ alisema (Mwenye kutawadha akautengeza udhu wake, basi dhambi zake hutoka mwilini mwake mpaka hutoka chini ya kucha zake) [Imepokewa na Muslim.].
4.Huinua daraja
Amesema Mtume ﷺ (Je, siwaonyeshi nyinyi kile ambacho kwacho Mwenyezi Mungu hufuta dhambi na huinua daraja? Wakasema “Ndio, tuonyeshe” akasema: “Ni kueneza maji ya udhu kwenye viungo, na kukithirisha hatua za kwenga misikitini na kungojea Swala baada ya Swala. Hiyo ndiyo jihadi) [Imepokewa na Muslim.].



Comments
Post a Comment