Kuzuru Madina: fadhila zake na utukufu wake
Majina ya mji wa Mtume wa Madina
1. Madina:
Amesema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka {Wanasema: lau tutarudi Madina watawatoa walio watukufu zaidi wale walio wanyonge zaidi} [63: 8].
2. Twaba:
Amepokewa Jabir bin Samurah t akisema: « Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu(saw) akisema: (Hakika Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Ameipa Madina jina la Twaba) [Imepokewa na Muslim.].
3. Twayiba:
Amepokewa Zaid bin Tahabit t akisema kumpokea Mtume(saw): (Hiyo ni Twayiba, inaondoa dhambi kama ambapo moto unaondoa uchafu wa fedha) [Imepokewaq na Bukhari na Muslim.].
Fadhila za Madina ya Mtume
1. Sa›d bin Abii Waqqaasw t amepokewa akisema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: (Madina ni bora kwao lau walikuwa wanajua. Haiachi mtu yoyote kwa kutoipenda isipokuwa Mwenyezi Mungu humweka mtu bora kuliko yeye awe ni badala yake. Na yoyote atakayevumilia shida zake [ La’waa’: Shida na dhiki za maisha.] na usumbufu wake, nitakuwa ni muombezi wake au shahidi wake Siku ya Kiyama) [Imepokewa na Muslim.].
2. Abu Huraira t amepokewa akisema kwamba Mtume (saw) amesema: (Nimeamrishwa kwenye kitongoji [ Nimeamrishwa kwa kitongoji: nimeamrishwa nigurie hapo, niteremkie hapo na niishi hapo.] kinachokula vitongoji [ Kinachokula vitongoji: watu wake wata washinda watu wa miji mingine na kitakuwa ni kituo cha majeshi ya Kiislamu.], wanakiita Yathrib [ Wanakiita Yathrib: Watu wake walikiita Yathrib wakati wa jahilia, na sasa kinafaa kiitwe Madina.], nayo ni Madina, inawaondoa watu [ Kinawaondoa watu: Kinawatoa wabaya miongoni mwao.], kama vile kiriba [ Kiriba: ni kile kinachovuviwa na mfuzi wa chuma ndani ya moto.] kinvyoondoa uchafu wa chuma [ Uchafu wa chuma: uchafu wake na takataka zake.]) [Imepokewa na Bukhaeri na Muslim.].
Miongoni mwa mambo yanayo husu Mji wa Madina
1. Ni mji mtakatifu wa amani kuanzia eneo la ‘Ayr mpaka Thaur. nayo ni majabali mawili. miti yake haikatwi na wanyama wake hawawindwi.
Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: (Madina ni takatifu, kuanzia ‘Ayr mpaka Thaur. Basi yoyote mwenye kuzusha uzushi humo au akampa himaya mzushi, itamshukia yeye laana ya Mwenyezi Mungu, Malaika na watu wote) [Imepokewa na Bukhaeri na Muslim.].
Comments
Post a Comment