Maana ya Dhahabu na Fedha

Dhahabu na Fedha
Dhahabu na fedha, na chochote kinachosimamia nafasi ya vitu hivi viwili miongoni mwa pesa za karatasi zinazotumiwa siku hizi.

Hukumu ya Zaka ya Dhahabu na Fedha.

Ni lazima; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu U: {Na wale wanaokusanya dhahabu na fedha wala hawazitoi katika njia ya Mwenyezi Mungu, wape habari za adhabu inayoumiza } (At-Tawbah 34)
na kwa kauli ya Mtume ﷺ: ( Mtu yeyote aliye na hazina ya dhahabu na fedha na wala haitolei Zaka basi atachomwa nayo katika moto wa Jahannam na itajaaliwa kama vinoo ambavyo atapigwa navyo kwenye migongo na vipaji kila akipata ubaridi (yakipoa makali ya moto) anaregelewa tena (kupigwa navyo), mpaka Allaah Amalize kuhukumu waja wake siku ambayo ni sawa na miaka elfu khamsini. Kisha ndio ataoneshwa njia yake ikiwa kama ni ya peponi au motoni” [Imepokewa na Muslim.].

Masharti ya kuwajibika kutolewa kwa zaka ya Dhahabu na Fedha

1. Kupitiwa na mwaka.
2. Kuzimiliki kiukamilifu.
3. kufika nisabu ya zaka.

Nisabu ya zaka ya Dhahabu na Fedha

1. Nisabu ya dhahabu ni Dinari ishirini (85gms)
2. Na Dinari moja ya dhahabu = (ina dhahabu) gramu nne na robo, hivyo basi inakuwa nisabu ya dhahabu kwa gramu 4.25 x 20 = 85gms za dhahabu safi (ambayo haikuchanganywa na kitu).
3. Nisabu ya fedha ni Dirham mia mbili (595 gms)
Na Dirham moja ya fedha = (ina fedha) 2.975gms, hivyo basi inakuwa nisabu ya fedha kwa gramu = 2.975 x 200 = 595gms za fedha safi.
Mfano: Ikiwa gramu moja ya dhahabu = inauzwa Dolari 30, basi inamlazimu mtu kutoa zaka ikiwa amefikisha 85 x 30 = Dolari 2550 dolari.
 Dhahabu
 Fedha
 Pesa za karatasi

Comments

Popular Posts