makka na sehemu ya ibada ya hijja
Tarehe ya Makka na hali ilivyokuwa na ilivyo sasa
Ni jina linalotokana na neno (bakka) lugha ya Kisamia ambalo maana yake ni bonde
Neno la Makka pia limekuja kwa tamshi la Bakka katika neno la Mwenyezi Mungu : {Hakika nyumba ya kwanza iliyowekewa watu ni iliyo Bakka, hali ya kuwa ni yenye baraka na uongofu kwa viumbe wote} [3: 96].
Tarehe ya Makka inakwenda nyuma hadi karne ya kumi na tisa kabla ya kuzaliwa Mtume Issa u, katika kipindi cha bwana wetu Ibrahim na Ismail, amani ziwashukie, kwani walikuwa ni watu wa mwanzo wa kukaa hapo. Mwenyezi Mungu U Anasema, Akimtolea hikaya Ibrahim: {Mola wetu! Hakika mimi nimewakilisha watu wa nyumbani kwangu kwenye ardhi isiyokuwa na mazao, kwenye Nyumba yako tukufu, ewe Molawetu!, ili watekeleze Swala. Basi zifanye nyoyo za watu ziwaelekee wao kwa mapenzi na uwaruzuku matunda ili washukuru} [14: 37].
Na kwa fadhila ya dua ya bwana wetu Ibrahim u yalitembuka maji ya Zamzamu kutoka chini ya nyayo za Ismail u alipomalizikiwa na maji na chakula mama yake, Hajara. Na kutoka wakati huo, makabila yalikusudia kuja hapo kwenye maji, na mahali hapo pakaanza uhai.
Na makabila yakaendelea kuja hapo na kuzaana, mpaka utawala wa mahali hapo ukaja kwa Makureshi. Na Makureshi wakaendelea kutawala mpaka kudhihiri Nabii Mohammed(saw) ambaye alikuwa na athari kubwa zaidi katika kugeuza maisha ya Makka tukufu na ulimwenguni kote.
Comments
Post a Comment