Masharti ya kufanya Swala iwe sahihi


Kwanza: kuingia wakati

Swala ya faradhi ina wakati ambao haiswihi kabla yake, wala baada yake isipokuwa kwa dharura. Asema Mwenyezi Mungu aliyetukuka: { Hakika Swala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalum} [4: 103],
yaani imefaradhiwa katika vipindi maalumu.
Nyakati za Swala ni: .

1. Wakati wa Alfajiri:

Ni kuanzia kutoka alfajiri ya kweli, nao ni ule weupe unaokuwa kwenye pambizo upande wa Mashariki, mpaka kuchomoza jua.

2. Wakati wa Adhuhuri:

Ni kuanzia kupinduka jua mpaka kivuli cha kitu kiwe mfano wake, baada ya kile kivuli cha kupinduka jua. Hivyo ni kwamba jua likichomoza kitu kinachosimama huwa na kivuli upande wa magharibi, kisha kivuli hiko huenda kikipungua kila jua likipanda mpaka kivuli kisimame. Kisha kivuli kinaanza kuongezeka, na ongezeko hili lianzapo hua ndio wakati wa kupinduka.

3. Wakati wa Alasiri:

Ni kuanzia wakati wa Adhuhuri kuisha mpaka kivuli cha kitu kiwe ni mara mbili yake baada ya kivuli cha kupinduka jua.

4. Wakati wa Magharibi:

Ni kuanzia jua linapozama mpaka yapotee mawingu mekundu, nayo ni ule mwangaza mwekundu unaokuwa kwenye pembe za mbingu pale jua linapozama.

5. Wakati wa Isha:

Ni kuanzia kipindi cha Magharibi mpaka nusu ya usiku, kwa neno lake ﷺ: (Wakati wa Swala ya Isha ni mpaka usiku wa kati) [ Imepokewa na Muslim.].
Na katika zama hizi, inawezekana kujua nyakati za Swala kwa urahisi kwa njia ya kuweka jaduali za kujulisha nyakati.
 Swala ya Alfajiri
 Swala ya Adhuhuri
 Swala ya Alasiri
 Swala ya Magharibi
 Swala ya Isha
Yasiofaa
- Kuswali na nguo ya kubana yenye kusifu uchi wa mtu, au nguo nyembamba yenye kuonyesha, au kuswali na huku akiwa tupu yake inaonekana, au na isbaal nao ni mtu kuswali na nguo yake imevuka vi fundoni.
- Kuswali na nguo yenye picha, au kuswali sehemu zilowekwa picha za roho, au kuswalia mswala wenye picha na michoro.
- Kuswali katika Msikiti wenye Makaburi, kwa neno lake Mtume ﷺ (Jueni kuwa watu walio kuwa kabla yenu wakiyafanya makaburi ya manabii wao na watuwema wao misikiti, basi musiyafanye makaburi yeni misikiti mimi nawakataza hilo) [ Imepokewa na Muslim.]
Faida
1. Mwenye kuwahi rakaa moja kabla ya kutoka wakati huwa amewahi Swala, kwa kauli yake Mtume ﷺ: (Mwenye kuwahi rakaa moja ya Swala huwa amewahi Swala) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
2. Ni lazima kutekeleza Swala kwa haraka iwapo wakati wake umepita kwa kulala au kwa kusahau, kwa neno lake Mtume ﷺ: (Mwenye kuisahau Swala basi ni juu yake aiswali anapoikumbuka, hakuna kafara yake isipokuwa hiyo) [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Comments

Popular Posts