NAMNA YA SWALAH YA IJUMAA

Hukumu ya Swalah ya Ijumaa

Swalah ya Ijumaa ni wajibu kwa kila Muislamu, aliyebaleghe, asiye na udhuru wa kuiacha.
Dalili ya hilo:
1. Neno la Aliyetukuka: {Enyi mlioamini! Kukinadiwa Swala kwa siku ya Ijumaa, endeni kwa haraka kwenye utajo wa Mwenyezi Mungu, na muache biashara} [62: 9].
2. Neno la Mtume ﷺ: ( Hawatoacha watu kuhudhuria Ijumaa, au Mwenyezi Mungu Atapiga mihuri juu ya nyoyo zao, kisha wawe ni miongoni wa walioghafilika) [Imepokewa na Muslim].

Wale ambao Ijumaa si lazima kwao

Swala ya Ijumaa haimlazimu mwanamke, mtoto mdogo, msafiri na mgonjwa ambaye atadhurika akiihudhuria, lakini inasihi kwa wote hao. Wakihudhuria pamoja na wengine itawatosheleza na wakitohudhuria, wataswali Adhuhuri.
 Mwanamke
 Mtoto mdogo
 Mgonjwa
 Msafiri

Ubora wa siku ya Ijumaa

Siku ya Ijumaa ni bora ya siku za wiki ambayo Mwenyezi Mungu Amewahusu nayo Waislamu baada ya umma wengine kuwapotea. Na zimekuja hadithi nyingi kuhusu ubora wake, miongoni mwazo:
1. Neno lake Mtume ﷺ: ( Siku bora iliyotokewa na jua ni siku ya Ijumaa. Katika siku hiyo aliumbwa Adam, na katika siku hiyo alitiwa Peponi, na katika siku hiyo alitolewa humo) [Imepokewa na Muslim].
2. Amepokewa Abu Huraira t akisema kwamba Nabii ﷺ alisema: (Mwenye kuoga siku ya Ijumaa, akaswali alichokadiriwa kuswali, kisha akakaa kimya mpaka imamu akamaliza hutuba yake, kisha akaswali pamoja naye, atasamehewa dhambi zilizo baina ya siku ile na Ijumaa nyingine na nyongeza ya siku tatu) [Imepokewa na Muslim].
3. Amepokewa Abu Huraira t akisema kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alikuwa akisema: (Swala tano, na Ijumaa mpaka Ijumaa, na Ramadhani mpaka Ramadhani vinafuta dhambi zilizo baina yake, iwapo mtu atajiepusha na dhambi kubwa) [Imepokewa na Muslim].

Comments

Popular Posts