Nguzo, Wajibu na Sunna za Hija


Nguzo za Hijja

1. Kuhirimia:

kwa neno la Mtume (saw): ( Hakika matendo mema yategemea nia, na hakika kila mtu atapata lile alilonuilia) [Imepokewa na Bukhari.].

2. Kusai baina ya Swafaa na Marwah:

kwa neno lake (saw): (Saini, kwani Mwenyezi Mungu Amewafaradhia kusai) [Imepokewa na Ahmad.].

3. Kusimama Arafa:

kwa kauli ya Mtume (saw): (Hija ni Arafa) [Imepokewa na Tirmidhi.].

4. Twawafu ya Ifaadhah:

kwa neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: {Na ili waitufu Nyumba ya Zamani} [22: 29].
- Tanabahisho
Mwenye kuacha nguzo moja miongoni mwa nguzo za Hijja, ikiwa ni kuhirimia basi ibada yake haikubaliki kwa sababu hakutia nia na ibada haikubaliki bila ya nia na ikwa ni nguzo nyingine ya Hijja haitatimia mpaka ailete.

Wajibu za Hijja

1. Kuhirimia kwenye sehemu zilizowekwa kuhirimia:

kwa neno lake (saw) baada ya kuzitaja sehemu za kuhirimia: (Hizo ni za watu wa sehemu hizo na wale wanaokuja hapo kati ya watu wa sehemu nyingine miongoni mwa wale wanataka kuhiji au kufanya Umra) [Imepokewa na Bukhari].

2. Kusimama Arafa mpaka jua kuzama kwa aliyesimama mchana:

Kwa kuwa Nabii (saw) alisimama mpaka jua likazama.

3. Kulala hapo Muzdalifa:

kwa sababu Mtume (saw) alilala hapo na akasema: (Umma wangu wachukue ibada yao ya Hija kutoka kwangu, kwani mimi sijui pengine huenda nisikutane nao baada ya mwaka wangu huu) [Imepokewa na Ibnu Maja.].
Na kwamba yeye (saw) aliwaruhusu Waislamu madhaifu baada ya nusu ya usiku. Hilo linaonyesha kwamba kulala hapo Muzdalifa ni lazima. Na Mwenyezi Mungu Ameamrisha atajwe katika Mash’ar al-Haraam.

4. Kulala Mina masiku ya siku za tashriiq:

kwa ilivyothubutu kwamba Nabii (saw) aliwaruhusu wachungaji kulala kando ya Mina [Imepokewa na Abu Ya›laa katika Musnad yake.].
Hii inaonyesha kwamba asili ni kuwa kulala Mina ni wajibu.

Comments

Popular Posts