nusuk na Talbiya
Ibada ya Hijja (nusuk)
Maana ya Ibada ya Hija (nusuk)
Ibada
Ni maneno yanayosemwa na vitendo vinavofanywa na Mwenye kuhiji au kufanya Umra.
Nia ya ibada ya Hijja (nusuk)
Anapomaliza kuoga na kujinadhifisha yule anayetaka kuhirimia, akavaa nguo za ihramu, na mwanamume akatoa nguo za mzunguko, atanuilia kuingia kwenye ibada ya Hijja au Umra.
Na inapendekezwa aitamke aina ya ibada anayoikusudia. Aseme akikusudia Umra kisha kujistarehesha mpaka Hijja: «LABBAYKA ALLAHUMMA UMRATAN MUTAMATIAN ILAA-L HAJJI Nakuitikia, ewe Mola, kwa kufanya Umra hali ya kujipumzisha nayo mpaka nifanye ibada ya Hijja» au aseme: LABBAYKA ALLAHUMMA UMRATAN «Nakuitikia kwa kufanya Umra» kisha wakati wa Hijja aseme: LABBAYKA ALLAHUMMA HAJJA «Nakuitikia kwa kuhiji». Na mwenye kuzishikanisha pamoja Hijja na Umra»Nakuitikia kwa Hijja na Umra».
Kwa hadithi ya Anas t kuwa alisema: (Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema: ”Nakuitikia Kwa kuhiji na kufanya Umra”) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Na asipotamka chochote nia ya moyoni inamtosheleza.
Comments
Post a Comment