Nyakati (mawaaqiit)
Maana ya miiqaat
Kuweka mpaka baina ya vitu viwili.
Ni mipaka iliyowekwa na sharia kwa ajili ya ibada na yawakati na Namahali.
Aina ya nyakati
Kwanza: Nyakati za mahali
Ni sehemu zilizowekwa na Sheria kuhirimia kutoka hapo
Haifai kwa anyetaka kuhiji au kufanya Umra azipite sehemu hizo isipokuwa awe amehirimia. Nazo ni sehemu tano [Al-Mawaaqiit wa Ab›aaduhaa. Sheikh Abdullah Al-Bassaam, Gazeti la Majma’ al-Fiqh al- Islaami, Idadi: 3, Juzu: 3, ukurasa 1553]:
1. Dhul Hulaifah
Nayo ipo upande wa kusini wa mji wa Mtume wa Madina, na unaitwa «Abyaar ‹Ali». Iko mbali na Makka kwa masafa ya kilimita 420.
Nayo ni mahali pa kuhirimia watu wa Madina.
Dhul Hulaifah
2. Juhfah:
Nayo iko karibu ya mji wa Raabigh, na ina umbali wa kiasi cha kilomita 186 kutoka Makka.
Nayo ni mahali pa kuhirimia watu wa Shaam, Masri na nchi za upande wa maghribi
Juhfah
3. Yalamlam:
Nayo ni bonde kubwa kwenye njia ya watu wa Yaman kwenda Makka.
Kwasasa inaitwa: Assa›diyyah, na iko mbali na Makka kwa kiasi cha kilomita 120.
Nayo ni mahali pa kuhirimia watu wa Yaman.
Comments
Post a Comment