Sadaka ya kujitolea
Maana ya sadaka ya kujitolea
Ni kinachotolewa kwa lengo la kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu pasina kuwa ni lazima.
Na kwa maana hii inatolewa zawadi na mfano wake kuwa ni katika mambo yanayotolewa kwa lengo la kuzidisha mapenzi, hivyo basi vitu hivi haviingii katika vinavyoitwa sadaka maalumu zilizowekwa na hukumu za sheria.
Hukumu ya sadaka ya kujitolea
Sadaka ya kujitolea ni yenye kupendekezwa kwa wakati wowote ule, na hasaa ikiwa ni wakati unaohitajia kitu, na imehimizwa katika Qur’an na sunnah ya Mtume ﷺ miongoni mwayo ni:
- Maneno ya Mwenyezi Mungu U: {Ni nani atakaye mkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema ili Mwenyezi Mungu Amzidishie mzidisho mwingi} (Al-Baqarah: 245).
- Kutoka kwa Abu Hureirah radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie asema: Amesema Mtume ﷺ: (Atakayetoa sadaka ya tende nzuri alizozichuma kwa kichumo kizuri cha halali – na Mwenyezi Mungu hakubali ila kizuri – hakika Mwenyezi Mungu anakubali sadaka hii kwa Mkono wa kulia, kisha anamkuzia mwenyewe, kama vile anavyokuza mmoja wenu ndama wa farasi wake – mpaka inakuwa mfano wa jabali) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
- Mtume ﷺ amemuhisabu mwenye kuficha sadaka anayotoa miongoni mwa watu saba watakao finikwa na kivuli cha Mwenyezi Mungu, siku ambayo hakuna kivuli isipokua kivuli Chake (Na mtu aliyetoa sadaka akaificha, hata mkono wake wa kushoto usijuwe kilichotolewa na mkono wa kulia) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
- Na kutoka kwa Ka’b Ibn u’jrah radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie kwamba Mtume ﷺ amesema: (Na sadaka zinafuta madhambi kama maji yanavyozima moto) [Imepokewa na Tirmidhi.].


Comments
Post a Comment