Tarekh ya mitume:Issaa
Tarekh ya mitume:Issaa
Maryam ('Alayha salaam)
Baba yake Maryam (‘Alahyi Salaam) alikuwa ni ‘Imran, mja miongoni wa waja wa Bani Israil, alitokana na kizazi cha Dawud (‘Alahyi Salaam), katika nyumba ya wacha-Mungu, mama yake Maryam alikuwa hashiki mimba, akatamani kupata mtoto; akaweka nadhiri kwa Allah kuwa akipata mimba atamtoa mwanae wakfu kuitumikia dini na msikiti mtukufu (yaani mpenzi katika nyumba tukufu): “Alipo sema mke wa Imran: Mola wangu Mlezi! Nimekuwekea nadhiri kilichomo tumboni mwangu kuwa wakfu; basi nikubalie. Hakika Wewe ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua. Basi alipo mzaa alisema: Mola wangu Mlezi! Nimemzaa mwanamke - na Mwenyezi Mungu anajua sana aliye mzaa - Na mwanamume si sawa na mwanamke. Na mimi nimemwita Maryamu. Nami namkinga kwako, yeye na uzao wake, uwalinde na Shet’ani aliye laaniwa.” (3:35-36);
Allah akamkubalia mama yake Maryam nadhiri yake: “Tena Mola wake Mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema…” (3:37)
Katika sura nzuri na mandhari ya furaha na njia ya waja wema wenye furaha; na hivyo basi Allah akasema: “…na akamfanya Zakariya awe mlezi wake…” (3:37)
Allah akamneemesha kwa mlezi wake ni nabii vile vile, inasemwa kuwa alikuwa ni mume wa mama yake mdogo au mume wa dada yake: “…Kila mara Zakariya alipo ingia chumbani kwake alimkuta na vyakula. Basi alimwambia: Ewe Maryamu! Unavipata wapi hivi? Naye akasema: Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.” (3:37)
Ukarimu na utawala wa Allah kwake yeye, hivyo Mola wake akamkirimu, kumchagua, kumtoharisha, kumkamilisha na kumuamrisha kumuabudu: “Na angalia pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Kwa hakika Mwenyezi Mungu amekuteuwa, na akakutakasa, na akakutukuza kuliko wanawake wote. Ewe Maryamu! Mnyenyekee Mola Mlezi wako na usujudu na uiname pamoja na wainamao.” (3:42-43),


Comments
Post a Comment