Tarekh ya mitume:Musa

Tarekh ya mitume:Musa

Kuuliwa kwa watoto wa kaumu ya Musa

Bani Israil walikuwa wakisomeshana wenyewe kuhusiana na Mtume Ibrahim (‘Alahyi Salaam) kuwa katika kizazi chake atatoka kijana ambae mfalme wa Misri ataangamia kwa mikono yake, utabiri huu ulikuwa ni maarufu kwa Bani Israil. Habari zile zikafika kwa Firauni na maamiri wake walimueleza habari hiyo, hivyo kuamuru kuuwawa kwa wavulana wa Bani Israil kwa kutahadhari na kuwepo kwa kijana huyo. Zama hizo Bani Israil walikuwa wanaishi kwa kuonewa shida na dhuluma kubwa kutoka kwa Firauni: “Hakika Firauni alitakabari katika nchi, na akawagawa wananchi makundi mbali mbali. Akalidhoofisha taifa moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wanaume na akiwaacha watoto wao wanawake. Hakika yeye alikuwa katika mafisadi.” (28:4)
Allah akataka kuwaneemesha waliodhoofishwa miongoni mwa Bani Israil: “Na tukataka kuwafadhili walio dhoofishwa katika nchi hiyo na kuwafanya wawe waongozi na kuwafanya ni warithi. Na kuwapa nguvu katika nchi, na kutokana na wao kuwaonyesha kina Firauni na Hamana na majeshi yao mambo yale waliyo kuwa wakiyaogopa.” (28:5-6).

Kisa cha kuzaliwa na kukua kwake

Pamoja na Firauni kujihadhari na kukwepa kutopatikana Musa, kiasi cha kuwafanya askari wake wakiwazungukia wenye mimba na wakijua tarehe za kuzaa kwao, hivyo basi alikuwa hazai mwanamke yoyote mtoto wa kiume isipokuwa watamchinja wachinjaji hao muda ule ule, Lakini Allah alitaka kumuoneshe Firauni, Hamana na majeshi yake walichokua wakitahadhari. Pindi mama yake Musa alipozaa: “Tulimfunulia mama yake Musa kwa kumwambia: Mnyonyeshe. Na utakapo mkhofia basi mtie mtoni, na usikhofu wala usihuzunike. Hakika Sisi tutamrudisha kwako na tutamfanya miongoni mwa Mitume.” (28:7)
Hivyo akawa na khofu juu yake, akamuweka katika sanduku la mbao na kumtupa mtoni:“Basi wakamwokota watu wa Firauni, aje kuwa adui kwao na huzuni. Hakika Firauni na Hamana na majeshi yao walikuwa wenye makosa.” (28:8).

Comments

Popular Posts