Zaaka hukumu yake na masharti yake
Maana ya zaka
Ni kukua kwa kitu na kuzidi.
Ni kiwango maalumu cha mali kinachotolewa wakati maalumu ili kupewa watu maalumu.
Umuhimu wa zaka
Zaka ni faradhi katika faradhi za Dini ya Kislamu, na ni nguzo ya tatu katika nguzo za Uislamu, Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na simamisheni swala na toeni zaka} (Suratu An-Nur: 56),
Na akasema Mtume (saw): (Umejengwa Uislamu kwa mambo matano: Kushuhudia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja wake na ni Mtume wake, na kusimamisha Swala (tano za kila siku), na kutoa Zaka, na kuhiji nyumba tukufu (Al-ka’abah – ilioko Makkah), na kufunga Mwezi wa Ramadhani) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
Hukumu ya anayekataa kutoa Zaka.
Anayekataa kutoa Zaka, ima amekataa kwa kupinga kwamba sio lazima kutoa [Juhuud: Ni kukataa kuwajibishwa kwake.], au kwa ubakhili.
1. Mwenye kukataa kutoa Zaka kwa kupinga.
Anayepinga wajibu wa Zaka basi amekufuru kwa makubaliano ya umma wote – ikiwa mtu huyu anajua vizuri wajibu wa Zaka; kwa sababu atakuwa amemzulia uwongo Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
2. Anayekataa kutoa Zaka kwa ubakhili.
Atakayekataa kutoa Zaka kwa ubakhili wake basi huchukuliwa kutoka kwake Zakaa kwa nguvu na wala hawi kafiri kwa kufanya hivyo kukataa kutowa Zaka kwa ubakhili.
Na atakuwa ametenda dhambi kubwa miongoni mwa madhambi makubwa na ni uovu mkubwa sana.
Kwa kauli ya Mtume (saw) kuhusu wanaokataa kutoa Zaka: “Mtu yeyote aliye na hazina ya dhahabu na fedha na wala haitolei Zaka basi atachomwa nayo katika moto wa Jahannam na itajaaliwa kama vinoo ambavyo atapigwa navyo kwenye migongo na vipaji kila akipata ubaridi (yakipoa makali ya moto) anaregelewa tena (kupigwa navyo), mpaka Allaah Amalize kuhukumu waja wake siku ambayo ni sawa na miaka elfu khamsini. Kisha ndio ataoneshwa njia yake ikiwa ni ya peponi au motoni” [ Imepokewa na Bukhari.]


Comments
Post a Comment