ZAKA NA HUKMU YAKE KATIKA UISLAMU





wasifu
Maana ya ibada katika sheria ya Kiislamu ni mapana na inaingia ndani yake kila jema la kidini na la kidunia. Hakika ya ibada ni jina linalokusanya maneno na matendo yote Anayoyapenda Mwenyezi Mngu na kuridhika nayo. Muislamu katika dunia hii anajua kikweli kuwa yeye ni mja wa Mwenyezi Mngu uja wa kikweli. Anajighulisha kufikia uja huo kama inavyotakiwa ili awe ni mja wa kikweli wa Mola wake. Utukufu wake na ubora wake ni kuwa mja wa Mwenyezi Mngu, akufuata amri Zake na kujiepusha na makatazo Yake katika kila mamabo ya Dini yake na dunia yake.

Allah (Subhaanahu wa Taala) kwa hikma yake amewakunjulia baadhi ya waja riziki na wengine akawabania, na sio dalili ya kupendwa na Mwenyezi Mungu ukiwa umekunjuliwa riziki wala sio kuchukiwa ikiwa umebaniwa riziki. Kwani siku ya kiyama atakayenufaika ni atakayekuwa na moyo uliosalimika na maovu na ukiwa umeneemeshwa na Mola kwa kupewa mali, basi Allah amekupa mtihani kwa kukulazimisha utoe zaka ili kukuangalia utashukuru kwa kutekeleza amri yake ama utafanya ubakhili wa kutotoa zaka.
Kubainisha namna ya Mwenyezi Mungu Alivyotofautisha Waja wake katika Riziki
Enyi watu mcheni Mungu haki ya kumcha. Enyi waja wa Mwenyezi Mungu, miongoni mwa hikma za Mungu ni vile alivyo tofautisha tabia za watu na riziki zao. Amewakunjulia watu wengine na amewabania watu wengine na yote hayo ni kwa hikma yake Allah. Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala) katika Qur’an Tukufu:
قال الله تعالى : ((فَأَمَّا الْإِنْسَانُ إِذَا مَا ابْتَلَاهُ رَبُّهُ فَأَكْرَمَهُ وَنَعَّمَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَكْرَمَنِ15 وَأَمَّا إِذَا مَا ابْتَلَاهُ فَقَدَرَ عَلَيْهِ رِزْقَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَهَانَنِ 16) [الفجر: 16]
{{Pindi binaadam anapoonjwa na Mola wake na akamtukuza na akampa neema zake basi husema binaadam, Mola wangu amenitukuza, na pindi anapo muonja Mola wake na kumbania riziki yake basi husema, Mola wangu amenitweza. Sivyo hivyo}} [fajri 15-17].
Yaani sio kila aliyepewa ndio amependwa na wala sio kila aliyenyimwa huwa amechukiwa, bali hapa duniani, Mungu humpa amtakaye na humnyima amtakaye kwa hikma anayo ijua yeye mwenyewe ili kuangalia shukrani ya tajiri na subira ya maskini, kwani mali ni balaa kwa wengine na ni neema kwa wengine. Mwenye kujua ya kuwa kuna haki ya Mwenyezi Mungu katika mali yake, basi kwa mtu huyo mali kwake huwa ni neema, na ukisahau na mali ikawa ni sababu ya kupotea, basi mali itakuwa ni balaa kwako na mali itakuwa ni sababu ya kuadhibiwa kwa mtu huyo. Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala) katika Qur’an Tukufu:
قال الله تعالى) : فَلَا تُعْجِبْكَ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُمْ إِنَّمَا يُرِيدُ اللَّهُ لِيُعَذِّبَهُمْ بِهَا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَتَزْهَقَ أَنْفُسُهُمْ وَهُمْ كَافِرُونَ ) [التوبة: 55]
{{Yasikushangaze mali na watoto wao, hakika si jingine ila anataka kuwaadhibu kwa mali hayo katika uhai wa duniani na iwatoe roho zao hali ya kuwa ni makafiri}}.
Na Allah anatuambia kuhusu nabii wake Suleiman alipo muelimisha aliyo muelimisha na akaona neema ya Mungu juu yake. Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala) katika Qur’an Tukufu:
قال الله تعالى) : هَذَا مِنْ فَضْلِ رَبِّي لِيَبْلُوَنِي أَأَشْكُرُ أَمْ أَكْفُرُ) [النمل: 40] {{Hii ni fadhila ya Mola wangu ili apate kunifanyia mtihani kama nitashukuru ama nitakufuru}}. kinyume na aliyeghurika na akasema:
وقال: (إِنَّمَا أُوتِيتُهُ عَلَى عِلْمٍ عِنْدِي(. [القصص: 78]
{{Hakika si jingine, nimepewa kwa ajili ya elimu niliyonayo}}
Uwajibu wa Zaka na kuwa ni Nguzo katika Uislamu.
Ewe Muislamu Allah amewajibisha matajiri haki katika mali zao kuwapa maskini {Na wale katika mali zao kuna haki inayojulikana kwa wenye kuomba na wale walionyimwa}
Ili matajiri wawakunjulie ndugu zao maskini, na Allah Akafanya zaka ni nguzo ya tatu katika nguzo za Uislamu, kama alivyotuambia Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam): [Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano, kushuhudia ya kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) ni Mtume wake, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kufunga mwezi wa Ramadhani na kwenda kuhiji]. Amepokea hadithi hii Bukhari kutoka kwa Ibnu ‘Umar. Na katika swahihi mbili kutoka kwa Ibnu ‘Abbas radhi za Mungu ziwe juu yao amepokea 
neno la Mtume kumwambia Mu’adhi : [Wajulishe ya kuwa Allah (Subhaanahu wa Taala) Amewafaradhia Sadaka juu yao na inachukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kurudiswa kwa maskini wao]. Na dalili nyingi zimeeleza kuhusu zaka na umuhimu wake.
Ni nini Hikima ya Kufaradhishwa Zaka?.
Katika kufaradhishwa kwa zaka kuna hikma nyingi ambazo Allah (Subhaanahu wa Taala) Ameweka ndani yake. Kwanza ni kuusafisha moyo kutokana na ubakhili na kusafisha mali kutokana na uchafu kisha kutia baraka katika mali. Na kutoa zaka ni kuvunja nguvu za shetani kwani ukitoa zaka hutia nguvu imani kwa sababu huwa umeshinda hawaa yako na matamanio yako na wasiwasi wa shetani. Kwa sababu Allah (Subhaanahu wa Taala) Atwambia:
قال الله تعالى) : الشَّيْطَانُ يَعِدُكُمُ الْفَقْرَ وَيَأْمُرُكُمْ بِالْفَحْشَاءِ وَاللَّهُ يَعِدُكُمْ مَغْفِرَةً مِنْهُ وَفَضْلًا وَاللَّهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ) [البقرة: 268

Comments

Popular Posts