Zaka ya Mali ya biashara
Maana ya Mali ya biashara
Kila kilichoandaliwa kwa lengo la kuuzwa na kununuliwa ili mtu apate faida.
Ziliitwa hivi, kwasababu hazidumu, bali hutokeza na kupotea, kwani mfanyi biashara huwa hataki hizi bidhaa ki-uhakika, bali anataka faida ya pesa.
Na bidhaa za biashara zimekusanya vitu vyote vya sampuli zote za mali ambayo sio pesa zinazotumika kununulia vitu, kama vile magari, nguo, vitambaa, vyuma, mbao, na vyenginevyo vilivyoandaliwa kwa biashara.
Hukumu ya zaka ya Mali ya biashara.
Ni lazima; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu U: {Enyi mlioamini! Toeni katika vile vizuri mlivyovichuma, na katika vile tulivyokutoleeni katika ardhi} (Al-Baqarah: 267).
Jumla ya wanavyuoni wametaja kwamba makusudio ya aya hii ni: Zaka ya mali ya biashara, na kwa kauli ya Mwenyezi Mungu U: {Chukua kutoka kwa mali zao sadaka} (At-tawbah: 103) , na mali ya biashara ni katika mali zilizo dhahiri, basi Kwa ajili hii ikawajibika kutolewa zaka.


Comments
Post a Comment