MATUNDA YA IMANI


MATUNDA YA IMANI

Anasema Allwah Mtukufu {Huoni Mwenyeezzi Mungu Alivopiga Mfano Wa Neno Zuri Ni Kama Mti Ulio Mzuri Asli Imejik’ita Ardhini Na Utanzu Wake Uku Mbinguni, Hutowa Vyakula Vyake Kila Mara Kwa Idhni Ya Mola Wake.} (Ibrahim: 24-25)
Na Miongoni Mwa Matunda Ya Imani Ni Kama Yafuatavyo:
1-Imani Ya Kweli Hutia Utulivu Na Raha Ya Nafsi Na Ukunjufu WA Kifua. Na Hili Linasadikisha Neno Lake Mwenyeezzi Mungu {Juwa Kwamba WA Penzi WA Mwenyeezzi Mungu Hawana Kicho Wala Hawatahuzinika} (Yunus 62)
2-Ni Kupata Waumini Upamoja Makhsusi Kutoka Wa Mwenyeezzi Mungu , Yaani Huwatoa Kwenye Giza Ka Ukafiri Na Shida Zake Kuwapeleka Kwenye Nuru Ya Imani Na Thawabu Zake
3-Kufaulu Kwa Kupata Radhi Za Allah Na Pepo Yake Aliyo Waandalilia Waumini Wake Wakikweli Kweli. Kasema Allah Mtukufu: { Mwenyezi Mungu Amewaahidi Wanaomuamini Wanaume Na Wanawake (Amewaahidi) Mabustani (Pepo) Zipitazo Mito Mbele Yake Kukaa Humo Daima, Na Makazi Mazuri Katika Mabustani Hayo Yenye Kudumu, Na Radhi Za Mwenyezi Mungu Ni Kubwa Zaidi. } (At-Tawba: 72)
4-Allwah Anawahifadhi Na Kuwakinga Vipenzi Vyake: {Hakika Mwenyezi Mungu Huwatetea Walio Muaamini} (Al-Hajj: 38)
Miongoni Mwahayo: Allwah Kumkinga Mtume Wake Muhammad (S.A.W) Katika Tukio La Kuhama Kwake Na Jinsi Allwah Alimuhifadhi Ibrahim (A.W) Alipotupwa Ndani Ya Moto.
Kumuamini Allwah Ni Uhusiano Baina Ya Mja Dhaifu Na Mola Wake, Kama Vile Mwenye Nguvu Naye Pia Umuomba Allwah.
5-Utukufu Katika Dini Na Uongozi Kwenye Hiyo Dini, Amesema Mwenyeezzi Mungu (S.W): {Na Tukawafanya Miongoni Mwao Maimamu Wanaoongoza Kwa Amri Yetu Walipo Subiri} (As-Sajda 24)
Hakuna Dalili Kubwa Ya Hilo Kuliko, Utawala WA Watu WA Dini Na Yaqini Juu Ya Allwah, Allwah Ameendleza Matukufu Yao Na Wao Wako Chini Ya Matabaka Ya Michanga, Miili Yao Imekosekana Lakini Athari Zao Na Habari Zao Ziko Kwenye Maisha.
6-Mapenzi Ya Allwah Kwa Waumini, Amesema Allwah: {Mwenyezi Mungu Anawapenda Nao Wanampenda} (Al-Maaida: 54)
Na Amesema Allwah Mtukufu: {Hakika Wale Walioamini Na Kufanya A’amali Mzuri (Mwenyezi Mungu) Atawapa Upendo} (Maryam: 96)
Uhayi Pasina Imani Ni Mauti Yasiyo Shaka... Mboni Pasina Imani Ni Up’ofu. Ulimi Bila Imani Ni Ububu. Mkono Bila Imani Ni Mlemavu.
7-Maisha Mazuri Ya Dunia Na Akhera, Allwah Mtukufu Amesema: {Yoyote Mwenye Kufanya Mema, Awe Mume Au Mke, Na Hali Yeye Ni Mwenye Imani Tutampa Maisha Mazuri Na Tutawajazi Malipo Yao Kwa Vyema Kuliko Walivo Fanya.} (An Nahl 97)
Basi Wako Wapi Wenye Kutafuta Maisha Mazuri Na Furaha?
8-Mapenzi Ya Allwah Kwa Muumin Na Mapenzi Ya Muumin Kwa Allwah, Anasema Allwah: {Mwenyezi Mungu Anawapenda Nao Wanampenda} (Al Maaida 54)
Yaani Anawapenda Na Anawawekea Mahaba Kwa Watu.
9-Kupata Bishara Nzuri Kwa Watu WA Imani Kwa Ukarimu WA Allwah Kwao .Allah Mtukufu Asema: {Wabashirie Waumini} (At Tawbah: 112)
Wala Hakutolewi Bishara Illa Kwa Jambo Kubwa, Athari Yake Ikadhihiri Juu Ya Ngozi Ndipo Ikaitwa Bishara Wala Hakuna Kikubwa Kuliko Rehma Ya Mwenyeezzi Mungu Na Radhi Zake Na Pepo Yake, Anasema Allwah: {Wabashirie Walioamini Na Wakafanya Mema Kwamba Wana Mabustani Yanayo Pita Chini} (Al Baqarah 25).
10-Imani Ni Sababu Ya Kuthubutu, Anasema Allah Mtukufu: { Wale Ambao Watu (Waliwatisha) Wakawaambia, Watu Wamewakusanyia, Waogopeni (Hilo) Likawazidishia Imani Na Wakasema Tosho Letu Ni Mwenyeezzi Mungu Alie Mwema Wakutegemewa } (Aal Imran 173)
Wala Hakuna Ambalo Ni Dalili Kubwa Ya Kuthubutu Huku Kuliko Yale Yaliyo Andikwa Na Tarikhi Kuhusu Mitume Na Maswahaba Na Waliofuatia Wao, Na Alie Kwenda Juu Ya Mwendo Wao.
11-Kufaidika Na Mawaidha, Anasema Allwah Mtukufu: {Basi Wakumbushe, Kukumbusha Kunawafaa Waumini} (Adhariyat: 55), Hawafaidiki Na Mawaidha ILA Watu WA Imani.
12-Amiweka Kheri Kwa Hali Zote Kwa Mwenye Imani, Katika Hali Ya Furaha Na Katika Hali Ya Dhiki, Kheri Huwa Ni Yenye Kuambatana Na Muumin: &"Ni Ajabu Mambo Ya Muumin Hali Zake Zote Kwake Ni Kheri Halipatikani Hili Ila Kwa Muumini, Akipata Mazuri Hushukuru Ikawa Kheri Kwake, Na Yakimsibu Madhara Husubiri Ikawa Kheri Kwake.&" (Imepokewa Na Muslim)

Comments

  1. Ahsante kwa mafunzo mazuri
    na vp kuhusu hivyo vitabu vinapatikanaje

    ReplyDelete
    Replies
    1. karibu sana kwenye tovuti yetu akhey
      na mm nakuwalika kushiriki kwenye semina ya
      🕋 Semina ya mtambue allah na kumamini 🕋
      ================================
      🆓 Kujisajili kwenye Link ya Ukurasa wa Semina:
      https://www.with-allah.com/sw/kusajili-katika-semina-ya-mtambue-allah-na-kumamini
      ================================
      ➡️Follow this link to join my WhatsApp Group la wanaume 👇

      https://chat.whatsapp.com/I6XntY2F44EJ8nzRP70lSG

      Group la wanawake 👇

      https://chat.whatsapp.com/FaILOx5PHoJJecijScKl6P

      ➡️ Kujisajili katika Chanel ya Telegram: t.me/al_feqh_com_sw
      ...............................................................................................................
      1- Kunapojificha kumuamini Allah na haja ya waja mafukara kwa mola wao mkwasi
      (https://www.with-allah.com/sw/kunapojificha-kumuamini-allah-na-haja-ya-waja-mafukara-kwa-mola-wao)2- maana na matunda ya kumuani Allwah na mitume yake
      (https://www.with-allah.com/sw/maana-ya-kumuani-allwah-na-hakika-yake1)3- Maana ya (arrabu) Mola Mlezi na hoja juu ya juwepo
      (https://www.with-allah.com/sw/maana-ya-arrabu-mola-mlezi-na-hoja-juu-ya-juwepo)4- Maana ya Al-ilah (mwenye kuabudiwa) na fadhili ya la ilah ila Allah
      (https://www.with-allah.com/sw/maana-ya-al-ilah-mwenye-kuabudiwa-na-fadhili-ya-la-ilah-ila-allah)5- Kumpenda Allah, kutarajia na khofu
      (https://www.with-allah.com/sw/kumpenda-allah-kutarajia-na-khofu)6- Athari za ibada juu ya vitendo na tabia
      (https://www.with-allah.com/sw/athari-za-ibada-juu-ya-vitendo-na-tabia)7- Umuhimu wa kuyatambua majina ya Allah na sifa zake1
      (https://www.with-allah.com/sw/umuhimu-wa-kuyatambua-majina-ya-allah-na-sifa-zake1)8- Athari za kuamini majina na sifa zake Allah
      (https://www.with-allah.com/sw/athari-za-kuamini-majina-na-sifa-zake-allah)9- Kuishi pamoja na Allah na majina yake na sifa zake
      (https://www.with-allah.com/sw/kuishi-pamoja-na-allah-na-majina-yake-na-sifa-zake)10-Imani kamili na matunda yake (https://www.with-allah.com/sw/imani-kamili-na-matunda-yake)

      Delete

Post a Comment

Popular Posts